Ibada ya maombi kwa wanafunzi 21 walioangamia kwenye mksasa wa moto katika shule ya Hillside Endarasha Academy, iliyoratibiwa kuandaliwa Jumatano hii imeahirishwa hadi Alhamisi wiki hii.
Serikali awali ilikuwa imetengaza kuwa ibada hiyo ingeandaliwa katika uwanja wa Mweiga siku ya Jumatano, lakini kutokana na sababu ambazo haijataja, imehiari kusongeza mbele kwa simu moja.
Kaimu Kamishna wa kaunti ya Nyeri Pius Murugu amethibitisha kuwa hafla hiyo itaandaliwa katika uwanja wa Mweiga Alhamisi hii.
Moto mkali uliozuka katika bweni la shule hiyo tarehe 5 mwezi huu uliwateketeza wavulana hao waliokuwa wakilala.