Nyumba zaidi ya 5,000 kunufaika na mradi wa umeme Bungoma

Tom Mathinji
1 Min Read
Opiyo Wandayi - Waziri wa Nishati

Wizara ya Nishati imetoa shilingi milioni 600 kufanikisha mradi wa kuweka umeme kwa nyumba 5,400 katika kaunti ya Bungoma.

Akizungumza katika kijiji cha Lunakwe, kata ndogo ya Bumula,  Kaunti ya Bungoma, Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi alisema kuwa hii ni mojawapo ya miradi iliyotengewa shilingi bilioni 2.7 katika kaunti hiyo.

Aidha, Wandayi alidokeza kuwa kituo cha nishati cha Bumula kitagharimu shilingi milioni 60 katika hatua zake za awali na kitatumika kutoa mafunzo, huduma za nyanjani na katika maonyesho ya nishati mbadala.

Kulingana na Waziri huyo, wizara hiyo imetenga shilingi milioni 260 zitakazotumika kuweka umeme kwa nyumba 1,200. Kati ya pesa hizo, shilingi milioni 10 zitatumika kuweka umeme kwa makazi 132 katika kijiji cha Lunakwe.

Aliyasema hayo katika kijiji cha Lunakwe kaunti ndogo ya Bumula, kaunti ya Bungoma, alipozindua ujenzi wa kituo cha nishati cha Bumula.

Wandayi alidokeza kuwa huo ulikuwa mradi wa 17 kutekelezwa na wizara hio hapa nchini.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hio ni pamoja na Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka na mbunge wa Bumula Jack Wamboka.

Website |  + posts
Share This Article