Mageuzi katika idara ya magereza yanazaa matunda, asema Murkomen

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen.

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kipchumba Murkomen amesema mageuzi katika idara ya magereza nchini yanazaa matunda.

Akizungumza Jumanne alipokutana na maafisa wa ngazi za juu kutoka idara ya magereza wakiongozwa na Katibu Salome Beacco, Murkomen alisema idadi ya wafungwa imepungua kutoka 64,000 hadi 60,000 katika muda wa mwaka mmoja uliopita.

Alidokeza kuwa mageuzi yataendelea kutekelezwa kuhakikisha wale wanaokamilisha vifungo gerezani wanachangia katika ukuaji wa jamii.

Waziri huyo alisema baadhi ya mageuzi hayo ni pamoja na ujenzi wa makazi bora ya wafanyakazi na wafungwa na kupunguza msongamano gerezani.

Aidha, alisema kupitia mashamba na karakana zinazomilikiwa na magereza,  kutakuwa na utoshelevu wa chakula na nafasi za ajira,  hivyo basi kusababisha idara ya magereza kujisimamia.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ulioandaliwa katika jumba la Harambee, ni pamoja na kamishna mkuu wa idara ya magereza Patrick Aranduh miongoni mwa wengine.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *