Mafuriko yaathiri familia 600 Tana Delta

Tom Mathinji
1 Min Read
Familia zaidi ya 600 zimeathiriwa na mafuriko Tana River,

Takriban 600 zimelazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuriko katika eneo la Tana Delta.

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu, vijiji sita vimeathiriwa na mafuriko hayo, kutokana na mvua kubwa inayoshuhudiwa.

Naibu Katibu Mkuu wa Shirika hilo anayeshughulika na mipango Joe Mbalu, aliyezuru eneo hilo, alisema wakazi hao sasa wanaishi kwenye kambi za muda.

“Tunasaidia familia hizo ambazo zimeathiriwa kwa kuzipatia chakula, blanketi na mitungi ya maji,” alisema Mbalu.

Maeneo mengi nchini Kenya kwa sasa yanashuhudia vipindi vya mvua, hali inayosababisha mito kujaa maji kupita kiasi na kusababisha mafuriko.

Mafuriko yanatarajiwa kushuhudiwa, familia zaidi zikiwa katika hatari ya kuathiriwa na usaidizi zaidi unahitajika.

Share This Article