Mahakama ya Kakamega imemnyima dhamana Afisa wa Polisi anayesimamia kituo cha polisi cha Lumakanda Wycliffe Kwendo, baada ya kubainika kuwa anaweza ingilia ushahidi kwenye kesi inamkabii ya dhuluma ya kimapenzi dhidi ya mtoto mwenye umri wa miaka 14.
Huku akikanusha mashtaka dhidi yake, upande wa mashtaka ulipinga kuachiliwa kwake kwa dhamana ukisema wadhifa wake unamweka katika nafasi nzuri ya kuhitilafiana na ushahidi.
Upande huo wa mashtaka uliambia mahakama kuwa, mshtakiwa huyo aliwatishia mashahidi akitumia bastola yake, wakati alipokuwa akikamatwa.
Mahakama ilithibitisha haki ya kupewa dhamana lakini ikasema haki hiyo inaweza kosa kutimizwa iwapo upande wa mashtaka utatoa sababu za kuaminika.
Hakimu Mkuu mkazi Dorcas O. Mac’andere alidokeza kuridhishwa kwamba mshtakiwa anaweza vuruga ushahidi, kutokana na wadhifa wake na ikizingatiwa kuwa mlalamishi na shahdi wanaishi eneo moja na mshtakiwa.
Afisa huyo anazuiliwa katika gereza la Kakamega, akisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi dhidi yake.