Kenya na Japani kutatua changamoto zinazodumaza miradi ya maendeleo

Mudavadi alisema mradi wa eneo maalum la kiuchumi la Dongo Kundu utapewa kipaumbele, kwa lengo la kuvutia uwekezaji, kuimarisha uzalishaji bidhaa na kubuni nafasi za ajira kwa vijana wa Kenya.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya na Japani kutatua changamoto zinazodumaza miradi ya maendeleo.

Kenya na Japani zinashirikiana kukabiliana na changamoto zinazodumaza utekelezwaji wa miradi ya maendeleo nchini Kenya.

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, alisema mradi wa eneo maalum la kiuchumi la Dongo Kundu utapewa kipaumbele, kwa lengo la kuvutia uwekezaji, kuimarisha uzalishaji bidhaa na kubuni nafasi za ajira kwa vijana wa Kenya.

Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, aliyasema hayo aliposhiriki meza ya mazungumzo na mshauri wa Waziri Mkuu wa Japani Uno Yoshimasa na Balozi wa Japani nchini Kenya Hiroshi Mtsuura Jijini Nairobi.

“Kwa miongo sita, urafiki kati ya Japani na Kenya umesababisha msingi dhabiti wa kuchochea maendeleo, uvumbuzi na kubuni fursa za kiuchumi,” alisema Mudavadi.

Aidha, mudavadi alisema mazungumzo yao yalipigia kurunzi ushirikiano katika sekta ya miundombinu, uchukuzi, nishati, maji, kilimo na afya.

“Kenya inakaribisha upanuzi wa ushirikiano wa pande mbili katika sekta ya usalama, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Japani wa Yen milioni 500 kwa mashua za kushika doria na vifaa vingine kwa kuimarisha usalama wa majini,” alidokeza Mudavadi.

Share This Article