Wasanii wakongwe wa muziki wa Bongo Fleva, wakiongozwa na Madee Ali ambaye ni mratibu wa Tamasha ya Miaka 30 ya Bongo Fleva, leo Novemba 26, 2026, wamewasili Kahama mkoani Shinyanga.
Nyota hao waanzilishi wa Bongo Fleva wako tayari kwa ajili ya kutoa burudani kesho, Novemba 27, katika Ukumbi wa Malex Hall, kuanzia saa moja usiku.
Madee ameambia wanahabari kwamba sababu ya kubadilisha Wasanii wanaotumbuiza katika kila tamasha ni kutoa nafasi kwa Wakongwe wengine wenye sifa za kushiriki, ili kila mmoja apate fursa ya kukutana na Mashabiki wake.
Kahama ndicho kituo cha saba cha ziara hiyo ya tamasha ya miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva, iliyozinduliwa rasmi katika huko Mlimani City jijini Dar es Salaam Julai 2026.
Tangu kuanzishwa kwake, tamasha hiyo imefanyika katika miji sita, ambayo Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Zanzibar na Mbeya, waandalizi wakidhamiria kufikia mikoa yote.
Waandaaji wameahidi burudani ya aina yake itakayowakumbusha mashabiki nyimbo zilizotamba na kuipa Bongo Flava utambulisho wake, sambamba na vibao vipya vinavyotikisa chati za muziki.