Kampuni ya Qatar kuwekeza shilingi Trilioni 2.6 hapa nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, ashiriki mazungumzo na waziri wa Ulinzi wa Qatar Dkt. Khalid bin Mohammed Al Attiyah,

Kampuni moja ya nchini Qatar, imeahidi kuwekeza hadi shilingi trilioni 2.6 nchini Kenya na katika kanda hii.

The Thirty-Five Group imesema kuwa hatua hiyo imetokana na ukuaji wa kiuchumi unaoshuhudiwa barani humu, na jukumu la Kenya kuwa kitovu cha kufanikisha mabadiliko katika uwekezaji.

Hayo yaliafikiwa Jumatatu kwenye mazungumzo kati ya Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia mudavadi na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni waziri wa Ulinzi Dkt. Khalid bin Mohammed Al Attiyah,

Katika mkutano huo ulioandaliwa Jijini Doha, viongozi hao wawili walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika uongozi, biashara na uwekezaji baina ya nchi hiyo mbili.

Dkt. Al Attiyah alielezea nia ya kupanua fursa zilizopo nchini Kenya na Afrika kwa jumla, akilenga maendeleo ya miundombinu, Kilimo na uvumbuzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

Mkutano huo ulijiri kabla ya ziara ya Rais William Ruto nchini Qatar, ambako anatarajiwa kuimarisha ushirikiano na taifa hilo la Kiarabu, na pia kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya Jamii.

Website |  + posts
Share This Article