Maafisa wa itifaki wa mabunge ya kaunti kupokea mafunzo ya kiusalama

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, amesema serikali inalenga kuwajumuisha maafisa wa itifaki na usalama wa  mabunge ya Kaunti katika makundi ya usalama ya kaunti na kuwapa mafunzo ya kijeshi.

Kulingana na Murkomen, hatua hiyo itawawezesha maafisa hao kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kulinda mabunge jayo.

“Kama wizara tunatambua kuwa usalama wa wabunge wetu kama wawakilishi wa wananchi ni muhimu kwa udhabiti wa taifa,” alisema Waziri Murkomen.

Akizungumza wakati wa  Mkutano wa tatu wa Kitaifa wa maafisa wa itifaki na usalama wa mabunge ulioandaliwa katika Kaunti ya Machakos siku ya Ijumaa, alisema usaidizi ulioratibiwa wa mashirika mbalimbali  kwa bunge na mabunge ya kaunti utaimarisha utulivu na udhabiti wa kitaifa.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Spika wa zamani wa bunge la Senate Ekwee Ethuro, Katibu wa Bunge la Taifa Samuel Njoroge, mwenzake wa Senate Jeremiah Nyegenye, na kiranja wa maafisa wa itifaki na usalama wa mabunge Meja Mstaafu Samson Sorobit.

Share This Article