Lissu ana kesi ya kujibu, mahakama yaamua

Aliambia Mahakama kwamba atajitetea mwenyewe.

Marion Bosire
1 Min Read
Tundu Lissu, Kiongozi CHADEMA

Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam nchini Tanzania, imetoa uamuzi leo na kusema kwamba mwenyekiti wa kitaifa wa CHADEMA Tundu. A. Lissu ana kesi ya kujibu.

Haya yanatokana na kesi ya uhaini ambayo imekuwa ikimkabili tangu mwezi Aprili 10, 2025.

Jaji Dunstan Ndunguru ndiye alisoma uamuzi wa jopo la majaji watatu ambao wamekuwa wakisikiliza kesi hiyo, wengine wakiwa James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Katika uamuzi huo, Jaji Ndunguru amesema baada ya kutathmini na kuzingatia ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hoja za mshtakiwa, wameona Lissu ana kesi ya kujibu.

Lissu anashtakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na Kifungu cha nambari 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, ya Tanzania iliyorekebishwa mwaka 2023.

Baada ya uamuzi huo kutolewa, Lissu aliambia Mahakama kwamba atajitetea mwenyewe baada ya Mahakama kuamua kuwa ana kesi ya kujibu katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Uamuzi huo umetolewa leo Agosti 21, 2026 na Lissu amesisitiza kwamba atatumia haki yake ya kujitetea na kwamba atajitetea mwenyewe kama Shahidi.

Madhila ya Lissu yanahusishwa na maneno anayodaiwa kutamka kuhusu kusudio la kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kupitia kwenye kampeni aliyokuwa akiendesha ya kuhimiza mabadiliko kabla ya uchaguzi.

Share This Article