Mahakama kuu ya Embu imeagiza kuhesabiwa tena kwa kura zilizopigwa mwenye eneo bunge la Mbeere Kaskazini wakati wa uchaguzi mdogo Mwezi Novemba mwaka jana.
Mahakama imesema hatua hiyo imechukuliwa kutoka na ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi huo mdogo, hitilafu za uhifadhi wa vifaa vya kupigia kura na kasoro kwenye sajili ya wapiga kura.
Kwenye matokeo ya uchaguzi huo, Leonard Wamuthende Njeru wa chama cha UDA alitangazwa mshindi huku akimshinda wa uchaguzi huo mpizani wake wa karibu Newton Kariuki wa chama cha Democratic Party of Kenya (DP).
Agizo hilo liliotolewa kwa njia ya kidijitali na jaji Richard Mwongo siku ya Ijumaa.
Jaji huyo aliitaka Tume Huru ya Uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC kuhakikisha shughuli ya kuhesabu upya kura na kuhakiki matokeo inafanyika.
Mlalamishi Newton Kariuki ameishtaki tume ya IEBC, John Mwii Kinyua, Curtis Njeru Mawira na Leonard Wamuthende Njeru, akidai kasoro kwenye kitambulisho chake na kwamba hakuwa amesajiliwa rasmi kama mpiga kura wakati wa uchaguzi huo.
Zoezi hilo litajumuisha uhakiki wa karatasi za kupigia kura, takwimu za vituo vya kupigia kura na vifaa vingine vya kupiga kura.
Matokeo ya shughuli hiyo yatabaini ikiwa mshindi anastahili au matokeo yaliyotangazwa yatafutiliwa mbali.