Mabarubaru wa Kenya, kujaribu kujizoa dhidi ya Tunisia leo AFCON U20

Morocco na Nigeria pia watapimana nguvu katika mechi ya pili ya kundi hilo kuanzia saa tatu usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya soka kwa wanaume walio chini ya umri wa miaka Rising Stars, itashuka dimbani  30th June, leo jioni kuanzia saa thenashara kupimana ubabe na Tunisia katika mechi ya pili kundini B kuwania kombe la AFCON.

Pande zote zinashiriki mechi hiyo zikilenga kurekebisha makosa katika mechi za ufunguzi ambapo Kenya, walipoteza 3-2 kwa Morocco, huku Tunisia wakilazwa 1-0 na Nigeria.

Kenya inayoshiriki kipute cha AFCON, kwa mara ya kwanza katika historia chini ya mfumo mpya wa mashindano watalenga kuepuka kupoteza mechi ya pili mtawalia ambayo itatia doa ndoto ya kufuzu kwa hatua ya mwondoano.

Morocco na Nigeria pia watapimana nguvu katika mechi ya pili ya kundi hilo kuanzia saa tatu usiku.

Katika matokeo ya mechi za jana za kundi A, wenyeji Misri walitoka sare kappa dhidi ya Zambia, huku Sierra Leone, ikiwa timu ya kwanza kufuzu kwa robo fainali baada ya kuibwaga Tanzania goli moja bila jawabu.

Timu nne bora kwenye mashindano hayo zitafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kati ya Septemba na Oktoba mwaka huu nchini Chile.

Website |  + posts
Share This Article