Koome achapisha rasmi uteuzi wa mahakimu zaidi ya 200

Dismas Otuke
1 Min Read

Jaji Mkuu Martha Koome amechaisha rasmi kwenye gazeti la serikali uteuzi wa mahakimu zaidi ya 200 kote nchini  kutatua kesi maalum.

 Mahakimu hao watafanya uamuzi wa kesi kuhusiana na usifadi,mazingira,mizozo ya ardhi,uajiri na mahusiano ya wafanyikazi pamoja na kesi za uhalifu wa kiuchumi.

Hii ni sehemu ya mageuzi katika idara ya mahakama nchini yanayolenga kuboresha utoaji huduma.

Mahakimu sita walijukumiwa kushughulikia kesi za ufisadi  na uhalifu wa kiuchumi wakiwa;Maureen Iberia, Victoria Achieng Ochanda, Janette Wandia Nyamu, Wilson Kipchumba Kitur, Christabel Irene Agutu na Japheth Cheruiyot Bii.

Mahakimu wengine 58 watasimia kesi za mazingira na mizozo ya ardhi.

Idadi nyingine ya Mahakimu 144 watashughulikia kesi za leba na uajiri.

Website |  + posts
Share This Article