Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, amejiunga na viongozi wengine ulimwenguni kumwomboleza Papa mtakatifu Francis, aliyeaga dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Uhuru amemtaja Papa Francis kuwa kiongozi aliyejitahidi kuunganisha madhehebu mbalimbali ya ulimwengu.
Uhuru ametaja ziara ya Papa humu nchini Novemba mwaka 2015, akisema ilihuisha imani ya Wakatoliki wengi.
Kifo cha Papa Francis kimetangazwa mapema leo na Kasisi Kevin Farrel Camerlengo ,nyumbani kwake Casa Santa Marta, akiwa na umri wa miaka 88.
Papa alionekana kwa mara ya kwanza hadharani jana tangu aanze kuugua, na amehudumu kwa kipindi cha miaka 12 afisini.
Makasisi 138 kati ya 258 wa kanisa Katoliki watashiriki zoezi la kupiga kura kumchagua Papa mpya.