Kombe la Dunia Wanawake: Uhispania yaiparuza Uholanzi na kutinga nusu fainali

Dismas Otuke
1 Min Read

Uhispania imejikatia tiketi ya kushiriki nusu fainali ya Kombe la Dunia kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uholanzi kupitia muda wa ziada, katika kwota fainali ya kwanza iliyosakatwa jana Ijumaa alfajiri katika uwanja wa Wellington Regional nchini New Zealand.

Uhispania iliyokuwa ikicheza robo fainali kwa mara ya kwanza ilimiliki mchuano huo kwa kipindi kirefu huku dakika 45 za mwanzo zikiishia sare tasa.

Kipindi cha pili, hali ilisalia ya mshike mshike kwa pande zote mbili lakini kunako dakika za lala salama, Waspanyola wakachukua uongozi kupitia penalti iliyovurumizwa kimiani na Marions Caldentey, baada ya Stefanie van der Gragt kuunawa mpira.

Hata hivyo, Van der Gragt alijitoa fedheha alipokomboa bao hilo na kufanya mechi kusakatwa kwa dakika 30 za ziada.

Hata hivyo, nguvu mpya Paralluelo alipachika goli la pili kunako dakika ya 111 lililodumu hadi kipenga cha mwisho na kuwapa Uhispania ushindi huku Uholanzi wakifunganya virago.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *