Kikosi cha Kenya kilichoshiriki mbio za Dunia mjini Guangzhou,China, kinatarajiwa kurejea nchini mapema kesho baada ya kuwahi tiketi tatu za mashindano ya Riadha Duniani Septemba mwaka huu.
Kenya ilizo nishani ya shaba katika mbio za mita 400, kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti mseto.
Aidha Kenya ilijikatia tiketi kwa mashindano ya Riadha Uliwenguni katika fani za mita 100 kwa wanariadha wanne wanaume, mita 400, kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti wanaume na mita 400 kupokezana kijiti mseto.