Kizo B atoka kizuizini

Mwanamuziki huyo alikuwa anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na umiliki wa ardhi. 

Marion Bosire
1 Min Read
Kizo B

Mwanamuziki Kizo B aliondoka kwenye gereza la Shimo la Tewa baada ya muda wa karibu wiki tatu.

B ambaye anafahamika sana wa wimbo wake “Ulinibeep” alikuwa anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na umiliki wa ardhi.

Makosa mengine yaliyotokana na hilo la kwanza ni kutishia mtu akitumia panga, madai aliyokanusha.

Baada ya kutiwa mbaroni, Kizo B alichapisha video ya kuomba usaidizi kutoka kwa umma akiwa rumande ambapo alielezea kwamba aliachiliwa kwa bondi lakini hakuwa na hela.

Alifafanua kwamba mashamba katika eneo la Pwani hayana hatimiliki na hilo ndilo lilimsababishia matatizo na mgogoro.

Kizo alisema mwaka 2027 alinunua shamba huko Mombasa akaamua kujenga nyumba na kuhamia huko.

Anasema aliyemuuzia shamba hilo ni mnyakuzi wa ardhi lakini hakujua.

Wafuasi wake mitandaoni walimwomba mtangazaji maarufu ambaye hujihusisha na wasanii Mzazi Willy M. Tuva amsaidie Kizo B.

Tuva na jamaa mwingine kwa jina Collins Muraya walifunga safari hadi Mombasa wakashughulika hadi akaachiliwa huru.

Baada ya kuachiliwa Kizo B alionekana mwenye furaha akisema, “Uhuru hatimaye! Dhoruba imekwisha na sura mpya inaanza.”

Alishukuru Mungu pamoja na  Tuva na Muraya. Watatu hao wameonekana kwenye video mitandaoni wakicheza densi kwa furaha.

Website |  + posts
Share This Article