Idara ya Takwimu ya Sudan imetangaza kuwa kiwango cha mfumuko wa bei kwa mwezi Septemba mwaka huu ni asilimia 215.52, ambacho kwa maeneo ya mijini kilikuwa asilimia 183.19 na maeneo ya vijijini ni asilimia 237.65.
Shirika la Fedha Duniani, IMF linatabiri kuwa mwaka huu, uchumi wa Sudan utaporomoka kwa asilimia 18.3.
Wakati huo huo, thamani ya sarafu ya Pound ya Sudan, inaendelea kushuka kwa kiasi kikubwa dhidi ya fedha za kigeni, na kusababisha kupanda kwa mfumuko wa bei.