Mashindano ya kuwania kombe la CECAFA kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 yatang’oa nanga Jumamosi katika kaunti za Kakamega na Kisumu.
Wenyeji kenya watapambana dhidi ya Sudan kundini A kuanzia saa tisa alasiri katika uga wa Mamboleo kaunti ya Kisumu .
Somalia watafungua dimba kundini A dhidi ya Rwanda saa sita Adhuhuri.
Kundi B litafungua mechi zake Jumapili uwanjani Bukhungu kaunti ya Kakamega ,Zanzibar wakichuana na Sudan Kusini kabla ya Tanzania kukabiliana na Uganda.
Mechi za makundi zitakamilika Disemba 2 kabla ya kupisha nusu fainali tarehe 5 mwezi ujao na fainali Disemba 8 katika uwanja wa Mamboleo kaunti ya Kisumu.
Mechi zote zitapeperushwa mubashara na runinga ya KBC Channel 1 na Y54 na kutangazwa kupitia Radio Taifa,Ingo FM na Mayienga FM.