Kenya yazindua huduma za upachikaji Figo katika hospitali ya KUTRRH

Tom Mathinji
1 Min Read
Hospitali ya Mafuzo na Rufaa ya Kenyatta yatoa huduma za upachikaji wa figo.

Kenya imezindua uduma za upachikaji wa figo katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta cha Mafunzo,  Rufaa na Utafiti, huku kikifanikisha upachikaji wa figo Mei 7 na 8, 2025.

Oparesheni hizo mbili za upachikaji wa figo zilifanikiwa, huku wagonjwa na waliotoa figo wakiwa katika hali dhabiti.

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa upachikaji wa figo siku ya Ijumaa, katibu wa idara ya huduma za matibabu Dkt. Ouma Oluga alidokeza kuwa maendeleo hayo yanaiweka Kenya kama kituo bora cha matibabu ya Figo nchini Kenya.

“Hatua hii inaashiria kujitolea kwa nchi hii kupanua huduma za matibabu hapa nchini na kupunguza utegemeaji wa matibabu kutoka nchi za nje,” alisema Dkt. Oluga.

Kuzinduliwa kwa kituo cha upachikaji Figo katika hospitali ya KUTRRH, kumetokana na juhudi kabambe zilizochukua muda wa miaka mitatu, ikiwa ni pamoja na utoaji mafunzo kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo.

Website |  + posts
Share This Article