Kenya Pipeline ndio timu pekee ya humu nchini iliyofuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Afrika kwa wanawake, mashindano yanayoendelea mjini Abuja, Nigeria.
Pipeline waliicharaza APR ya Rwanda seti 3-0 za 25-21, 25-17, na 25-14 katika kwota fainali ya jana na kulipiza kisasi cha kulemewa na APR katika mechi ya makundi.
Pipeline watashuka kucheza nusu fainali kesho jioni dhidi ya Zamalek walioibandua KCB seti 3-1, katika robo fainali jana Jumatano.
Nusu fainali ya pili itakuwa baina ya Carthage ya Tunisia dhidi ya Al Ahly ya Misri, baada ya Ahly kuwabandua Kenya Prisons seti 3-1 kwenye robo fainali ya jana.
KCB watamenyana na APR kuwania nafasi za 5 hadi 8 pia kesho o huku LTV ya Cameroon, wakimaliza udhia na Prisons ya Kenya.