Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula, amesema kenya itaendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Kenya na Uingereza.
Wetang’ula aliyasema hayo Alhamisi alipokutana na Balozi wa Kenya nchini Uingereza Maurice Makoloo.
Kwenye mkutano huo, spika huyo alisema waliangazia njia za kupiga jeki utekelezwaji wa sera zilizopo pamoja na kutoa uangalizi mwafaka.
“Wabunge hutekeleza jukumu muhimu la kujadili makubaliano, kuhakikisha yanawiana na malengo ya nchi,” alisema Wetang’ula.
Kulingana na Wetang’ula, ushirikiano kati ya Kenya na Uingereza unazingatia nguzo nne kuu, ambazo ni biashara, ukuaji wa kawi safi, Sayansi na Teknolojia, na Amani na Usalama.
Alisema Kenya inalenga kujifahamisha zaidi kuhusu akili unde kutoka kwa Uingereza.
