Kampuni ya uchukuzi wa ndege ya Uganda yazindua safari za London

Hii ni hatua kubwa kwa kampuni hiyo ya serikali ambapo ndege zake zitakuwa zikitua katika uwanja wa ndege wa Gatwick.

Marion Bosire
1 Min Read

Kampuni ya uchukuzi wa ndege nchini Uganda Uganda Airlines imezindua safari za moja kwa moja kuelekea London Uingereza.

Hii ni hatua kubwa kwa kampuni hiyo ya serikali ambapo ndege zake zitakuwa zikitua katika uwanja wa ndege wa Gatwick.

Safari hizo zitakuwa nne kila wiki huku ya kwanza ikitarajiwa Mei 18, 2025, kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe.

Hii ndiyo njia ya kwanza kabisa ya Uganda Airlines kuelekea Uingereza baada ya miaka kumi na inarejesha pia safari za moja kwa moja na UK.

Afisa mkuu mtendaji wa wa kampuni ya Uganda Airlines Jenifer Bamuturaki,alidhihirisha furaha yake kufuatia tangazo hilo akisema kwamba njia hiyo mpya itasaidia kampuni hiyo kupiga hatua katika kuafikia ukuaji na upanuzi.

Kulingana na Bamuturaki, kupata njia hii ya safari za ndege za moja kwa moja kati ya Uganda na London kulikuwa kazi ngumu na mashauriano yamedumu miaka mitano.

Mafanikio yangejiri mwaka 2020 lakini ujio wa janga la Covid 19 ukaathiri mipango.

Website |  + posts
Share This Article