Wenye hisa wa shamba la Chakama wajitenga na maafa ya Shakahola

Tom Mathinji
1 Min Read

Wenye hisa wa shamba la Chakama, ambako miili 338 ilifukuliwa, wamejitenga na maafa ya Shakahola katika kaunti ya Kilifi.

Akihojiwa na kamati inayochunguza maafa hayo, wakili wa wenye hisa hao Philip Kaingi alisema Paul Mackenzie alikuwa tu skwota kama watu wengine wengi kwenye ardhi hiyo na kamwe wateja wake hawajawahi kutangamana na mhubiri huyo.

Imebainika kwamba Mackenzie si mmiliki wa ardhi hiyo ambayo imekuwa chini ya usimamizi wa urasibu tangu mwaka 2016.

Kaingi alikuwa amefika mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Tana River Danson Mungatana ambayo inachunguza vifo vya Shakahola.

Tume ya kitaifa ya Kutetea Haki za Bbinadamu, KNCHR, shirika la Amnesty International pamoja na chama cha wanasheria nchini, LSK zimetoa wito wa kuwepo kwa uwajibikaji huku wapelelezi wakiendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha maafa ya Shakahola.

Hayo yanajiri baada ya kundi la watalaam na makachero kukamilisha awamu ya tatu ya ukaguzi wa miili iliyofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *