Watu kadhaa wahofiwa kunaswa ndani ya jengo lililoporomoka Westlands

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu kadhaa wanahofiwa kunaswa ndani ya jengo la ghorofa 22, lililoporomoka mtaani Westlands, kaunti ya Nairobi jana Jumatano jioni.

Watu hao wanaaminika kuwa wajenzi wa jengo hilo ambalo sehemu yake iliporomoka.

Taarifa kutoka kwa Shirika la Msalaba Mwekundu ilisema kuwa shughuli ya uokozi ingali inaendelea kwenye eneo la tukio.

Watu wawili kati ya wanne waliokuwa ndani ya jengo hilo walinusurika bila majeraha na kufanikiwa kuhepa huku wengine wawili wakiaminika kunaswa ndani yake.

Share This Article