Kalonzo na Sifuna wakutana, wasisitiza umuhimu wa umoja

Martin Mwanje
1 Min Read

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na yule wa vuguvugu la Linda Mwananchi Edwin Sifuna wamekutana mapema leo Alhamisi kujadili mustakabali wa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. 

Sifuna, ambaye pia ni Seneta wa Nairobi, amesema wakati wa mkutano wao, walikubaliana kwa kauli moja umuhimu wa wao kufanya kazi pamoja ili kuufurusha utawala wa sasa wa Kenya Kwanza madarakani.

Aidha, amesema walikubaliana juu ya umuhimu wa kurejesha demokrasia inayojikita kwenye katiba.

Wawili hao wamekutana wakati kukiwa na maswali chungu nzima ni nani kati yao atapeperusha bendera ya upinzani katika kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao ikiwa viongozi wa upinzani wataungana.

Wale wanaomshabikia Kalonzo wanataja tajriba ya miaka mingi katika uongozi ikizingatiwa aliwahi kuhudumu kama Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.

Wafuasi wa Sifuna, kwa upande mwingine, wanahisi analeta mwamko mpya kwenye siasa za Kenya.

 

 

Share This Article