Irungu Nyakera avuliwa uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KICC

Martin Mwanje
1 Min Read
Irungu Nyakera - Mwenyekiti anayeondoka wa Bodi ya Wakurugenzi wa KICC

Samuel Waweru Mwangi ndiye mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Jumba la Mikutano ya Kimataifa, KICC. 

Mwangi aliteuliwa na Rais William Ruto kuhudumu kwenye wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Rais Ruto alitangaza uteuzi huo kupitia gazeti rasmi la serikali liliochapishwa jana Jumanne.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, uteuzi wa Irungu Nyakera kama mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KICC umebatilishwa mara moja.

Awali, Nyakera alihudumu kama Mwenyekiti wa Shirika la Kusambaza Dawa nchini, KEMSA kabla ya kuhamishiwa KICC.

Nyakera aliteuliwa mwezi Agosti, 2024 kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KICC na alitazamiwa kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *