IMF: Azima yetu ni kuisadia Kenya kuzipiku changamoto za kiuchumi

Martin Mwanje
1 Min Read

Shirika la Fedha Duniani, IMF sasa linasema azima yake kuu ni kuisaidia Kenya kuzipiga dafrau changamoto ngumu za kiuchumi inazokabiliana nazo. 

Kadhalika, linasema linakusudia kuboresha uwezo wa kiuchumi wa taifa hili na hali ya maisha ya Wakenya.

“Tumesikitishwa mno na machafuko yaliyotokea nchini Kenya katika siku za hivi karibuni na kuhuzunishwa na vifo vilivyotokea na watu wengi kujeruhiwa,” alisema Julie Kozack ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa IMF.

“Mawazo yetu ni kwa watu walioathiriwa na machafuko nchini humo.”

IMF inasema imedhamiria kufanya kazi na Kenya kuelekea ukuaji thabiti wa kiuchumi ambao ni thabiti, endelevu na jumuishi.

Shirika hilo limekuwa likishutumiwa kwa kuwaweka masharti magumu kwa mataifa yanayostawi wakati likiyapatia mikopo ya kujiendeleza.

Ni masharti hayo yanayodaiwa kuwa chanzo cha machafuko katika mataifa hayo kwani yanafanya hali ya maisha kuwa ngumu hata zaidi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *