Historia yaandikishwa Kip Keino Classic

Dismas Otuke
1 Min Read

Historia iliandikishwa katika makala ya saba ya mashindano ya Kip Keino Classic,  yaliyoandaliwa Ijumaa usiku katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Mashindano hayo yalishuhudia rekodi mpya na muda wa kasi ukiandikishwa katika mashindano ya mbio na yale ya urushaji.

Kwa mara nyingine tena Ferdinand Omanyala  alitwaa taji ya mita 100, huku akiweka muda wake bora msimu huu wa sekunde 9.96,akiboresha muda wa sekunde 9.98, alioweka wiki jana katika mashindano ya Adidas Grandprix.

Bingwa wa Olimpiki Gabriella Thomas wa Marekani, alishinda mbio za mita 100 na mita 200,huku akiweka muda wake bora wa sekunde 21.89, katika mita 200.

Mercy Oketch alishinda mbio za mita 400 kwa sekunde 50.17,  akifuatwa na Paris Peoples wa Marekani, huku Mercy Chebet akikamilisha orodha ya tatu bora.

Bingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi alishinda mbio za mita 1500  kwa dakika 3 sekunde 34.11,akifuatwa na Timothy Cheruiyot, wakati Kyumbe Munguti akiridhia nafasi ya tatu.

Katika mashindano ya urushaji mabingwa wa Olimpiki Ethan Katzeberg na Camryn Rogers, walitwaa ubingwa huku wakiweka rekodi mpya.

Pia kwa mara ya kwanza teknolojia ya Wavelight ya kuwasaidia wanariadha kuongeza kasi ilitumika katika mashindano ya mwaka huu yaliyowashirikisha wanariadha zaidi ya 200 kutoka mataifa 37.

Share This Article