Harambee Starlets waripoti kambini kujiandaa kwa Morocco

Kenya wanalenga kufuzu kwa fainali za Afrika kwa mara ya pili tangu wafuzu mwaka 2016 kwa mara ya kwanza.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets, imeripoti kwa kambi ya mazoezi leo Jumapili, kujiandaa kwa mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Morocco tarehe 4 mwezi huu.

Wachezaji hao 23 wanaoongozwa na kocha mkuu Beldine Odemba, watatumia mchuano huo kujiandaa kwa mechi ya mwezi Oktoba, mwaka huu dhidi ya Gambia, kufuzu kwa fainali za kombe la Afrika mwaka ujao.

Kenya wanalenga kufuzu kwa fainali za Afrika kwa mara ya pili tangu wafuzu mwaka 2016, kwa mara ya kwanza.

Kikosi kilicho kambini

Makipa

Annedy Kundu, Vivian Shiyonzo

Mabeki

Leah Andiema, Phoebe Aketch, Dorcas Shikobe, Tabitha Amoit, Janet Mumo, Ruth Ingosi, Enez Mango, Vivian Nasaka,

Viungo

Diana Wacera, Martha Amunyolet, Sheril Angach, Fasila Adhiambo, Lavender Ann Akinyi, Corazone Aquino,

Washambulizi

Mwanahalima Adam, Violet Nanjala, Jentrix Shikangwa, Elizabeth Wambui, Faith Mboya, Emily Morang’a, Tumaini Waliaula

Website |  + posts
Share This Article