Agnes Ngetich, ashinda mbio za mita 3,000 mashindano ya Grand Slam Track

Jebet Ng'etich ametwaa ubingwa kwa kutumia muda wa dakika 8 sekunde 43.61

Dismas Otuke
1 Min Read

Agnes Jebet Ng’etich aliibuka mshindi wa mbio za mita 3,000 jana usiku katika  mashindano ya Grand Slam Track mjini Philadelphia,Marekani.

Jebet Ng’etich ametwaa ubingwa kwa kutumia muda wa dakika 8 sekunde 43.61 ,akifuatwa na Ejgayehu Taye kutoka Ethiopia ,kwa dakika 8 sekunde 43.70,huku  Andrews Josette wa Marekani, akiridhia nafasi ya tatu kwa dakika 8 sekunde 44.70.

Bingwa wa Dunia Mary Moraa alimaliza nafasi ya saba katika mbio za mita 1,500, kwa muda wa dakika 4 sekunde 1.70.

Deribe Welteji wa Ethioia aliibuka mshindi kwa kutumia dakika 3 sekunde 58.04.

Mashindano ya Slam yanashirikisha wanariadha bora kutoka ulimwenguni wanaoalikwa na kila mmoja anahitajika kushiriki mbio mbili.

Mshindi wa kila mzunguko  hutuzwa shilingi milioni 12.9 za Kenya,nafasi ya pili milioni 6.45, huku nambari tatu akiondoka na shilingi milioni 3.8 kuendelea hadi nafasi ya nane.

Jebet Ngetich aliibuka mshindi wa mashindano hayo mwezi April mwaka huu.

 

Website |  + posts
Share This Article