Gor Mahia wameambulia kichapo cha magoli matatu kwa nunge kutoka kwa mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri,katika duru ya kwanza ya mchujo wa pili kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili alasiri kiwarani Nyayo.
Percy Tao alipachika magoli mawili huku Rami Rabia akiongeza moja ,matokeo yaliyowaduwaza mashabiki wa nyumbani wakiongozwa na baadhi ya maafisa wa serikali.
Mabingwa wa Kenya watazuru Misri wiki ijayo kwa mchuano wa marudio wakihitaji muujiza wa ushindi wa mabao manne kwa nunge, ili kufuzu kwa raundi ya makundi.