Anderson Peters awasili Kenya, kwa Absa Kip Keino Classic

Peters atashindana na bingwa wa dunia mwaka 2015 Julius Yego wa Kenya .

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara mbili wa dunia katika urushaji sagai, Anderson Peters kutoka Grenada, amewasili nchini mapema leo kushiriki makala ya sita ya mbio za Absa Kip Keino Classic Continental Tour, Jumamosi hii Mei 31 katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex.

Peters ambaye alishinda nishani ya shaba ya Olimpiki mwaka jana, anarejea kushiriki Kip Keino Classic kwa mara ya pili baada ya kumaliza wa pili mwaka 2023.

Peter’s aliyeshinda nishani ya shaba ya Olimpiki mwaka jana alifungua msimu wake mwaka huu kwa kurusha umbali wa mita 85.64, katika mashindano ya Doha Diamond League tarehe 16 mwezi huu.

Ijumaa iliyopita alimaliza wa tatu kwa kurusha sagai umbali wa mita 83.24, katika mashindano ya Continental Tour ya Poland .

Peters atashindana na bingwa wa Dunia mwaka 2015 Julius Yego wa Kenya .

Jumla ya wanariadha 189 wametoa ithibati kushiriki, wakiwemo 130 wa kimataifa na 59 wa humu nchini.

Website |  + posts
Share This Article