Afrika Kusini imemteua mjumbe maalum kwenda Marekani katika juhudi za kupunguza mvutano unaoongezeka kati ya mataifa hayo mawili kufuatia kurejea kwa Donald Trump madarakani kama rais.
Rais Cyril Ramaphosa alimtangaza aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mcebisi Jonas, kama mjumbe, akieleza kuwa atakuwa na jukumu la “kuimarisha masuala ya kidiplomasia, kibiashara, na uhusiano wa pande mbili.”
Jonas anajulikana sana kwa hatua yake ya kufichua kashfa ya ufisadi inayomhusisha familia tajiri yenye uhusiano wa karibu na aliyekuwa Rais Jacob Zuma.
Uteuzi huu unakuja wiki chache baada ya Marekani kumfukuza Balozi wa Afrika Kusini, Ebrahim Rasool, kutokana na matamshi aliyotoa dhidi ya utawala wa Trump, hatua iliyozidisha mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.