Kenya kupimana ubabe na Nigeria,Tunisia na Morocco, AFCON ya mabarubaru

Timu mbili bora kutoka kila kundi na nyingine mbili bora za nafasi za tatu kutoka makundi yote matatu zitafuzu kwa robo fainali.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imepngwa kundi C pamoja na mabingwa mara saba Nigeria,Morocco na Tunisia, katika makala ya mwaka huu ya kipute cha kombe la AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20, kitakachoandaliwa jijini Cairo Misri kati ya April 27 na Mei  18 .

Droo hiyo iliandaliwa upya jana jioni jijini Cairo huku wenyeji Misri wakijumuishwa kundi A pamoja na
Zambia, Sierra Leone, Africa Kusini na Tanzania .

Mabingwa watetezi Seneagl wamerushwa kundi C pamoja na Jamhuri ya Afrika ya kati, DR Congo, na  Ghana.

Kundi  A: Egypt, Zambia, Sierra Leone, South Africa, Tanzania
Kundi B: Nigeria, Tunisia, Kenya, Morocco
Kundi C: Senegal, Central African Republic, DR Congo, Ghana

Timu mbili bora kutoka kila kundi na nyingine mbili bora za nafasi za tatu kutoka makundi yote matatu zitafuzu kwa robo fainali.

Timu nne bora katika mashindano hayo zitafuzu kwa fainali za kombe la Dunia kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 mwaka ujao nchini Chile.

Website |  + posts
Share This Article