Kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia kitaingia siku ya 14 Jumatano usiku kwa jumla ya mechi sita za kukamilisha ratiba ya makundi ya A, B na C .
Uswizi watakuwa mjini Vancouver Jumanne usiku katika mechi ya kundi B dhidi ya Wekundu wa Canada kuanzia saa nne usiku huku mshindi akiongoza kundi hilo, wakati Qatar ikimenyana na Bosnia Herzegovina mjini Seattle, Marekani ambapo mshindi atakuwa na fursa ya kufuzu kwa raundi ya 32 bora.
Atlas Lions ya Mororocco watapimana ubabe na Haiti uwanjani Atlanta saa saba usiku wa manane katika kundi C, Morocco wakiwania ushindi ili kuwa na uwezo wa kuongoza kundi hilo nao Brazil wakiwa na miadi na Scotland mjini Miami pia saa saba, mshindi akifuzu kwa hatua ya mwondoano.
Sare itawatosha Scotland na Brazil wote kufuzu kwa raundi ya 32 bora.
Baadaye, Mexio watahitimisha ratiba ya kundi A dhidi ya Czechia saa kumi alfajiri katika uwanja wa Mexico nao Korea Kusini wafunge kazi kwa wakati sambamba na Afrika Kusini.