Waziri wa afya Aden Duale amezindua usambazaji wa chanjo milioni tatu za BCG na nyingine milioni 3.2 za OPV, katika makao makuu ya wizara ya Afya mapema leo.
Akizungumza wakati wa kutoa chanjo hizo Duale, amezitaka serikali za kaunti kupitia kwa Baraza la Magavana kuhakikisha chanjo hizo zinasambazwa kwa wakati ufaao.
Waziri Duale aliandamana na Makatibu Mary Muthoni wa Afya ya umma, na Ouma Oluga wa huduma za matibabu.