FIFA U-17 Women’s World Cup:Kenya yaweka historia,huku Morocco ikidhihirisha miundo mbinu bora ya soka

Junior  Starlets ya Kenya ilifuzu kwa raundi ya 16 kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa ma mabao 4-0 dhidi ya Samoa katika mechi ya mwisho ya kundi E.

Dismas Otuke
2 Min Read
Uwanja wa michezo wa Mohammed Six mjini Rabat,Morocco

Timu ya Kenya kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 17, iliweka historia kwa kucheza hadi raundi ya 16 bora katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Morocco.

Junior  Starlets ya Kenya ilifuzu kwa raundi ya 16 kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa ma mabao 4-0 dhidi ya Samoa, katika mechi ya mwisho ya kundi E.

Uwanja wa Mohammed Six mjini Rabat,Morocco

Historia ya Kenya ni baadhi ya sehemu ya ufanisi wa Morocco kuandaa mashindano ya haiba kuu ambapo wachezaji wamepata fursa ya kudhihirisha vipaji.

Afrika iliwakilishwa na timu tano zikiwemo Zambia,Kenya,Nigeria,Ghana na wenyeji Morocco.

Fainali hizo zinashirikisha mataifa 24 ambayo kwa pamoja yatacheza jumla ya mechi 52 kushindania ubingwa.

Uwanja wa michezo wa Mohammed Six mjini Rabat,Morocco

Mechi hizo zimekuwa zikiandaliwa katika uwanja wa michezo wa Mohammed 6  jijini Rabat.

Kwa sasa bara lote la Afrika linajizatiti kugeuza ufanisi wa maandalizi kwa ukuzaji talanta wa muda mrefu.

Uwanja wa Mohammed Six mjini Rabat,Morocco

Haya yanajumuisha maendeleo ya wachezaji,kuimarisha vlabu,kukuza timu za taifa za wanawake na kukuza mashindano ya timu za taifa ili kudumisha viwango vilivyowekwa na Morocco kuwa viwango vya bara Afrika.

Share This Article