Wabunge wa EALA wataka kubuniwa kwa Viza moja ya wageni watakaohudhuria AFCON mwaka ujao

Uwanja wa Arusha umefikia asilimia 95 kukamilishwa ni mojawapo wa viwanja  sita vitakavyotumika kuandaa mechi za AFCON mwaka ujao .

Dismas Otuke
1 Min Read

Wabunge wa bunge la Afrika Mashariki ,EALA,wameweka shinikizo kubuniwa kwa stakabadhi moja ya Viza kwa watalii na wageni watakaosafiri kuhudhuria fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka ujao.

Fainali hizo za 36 zitaandaliwa kati ya Juni na Julai kwa pamoja na mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.

Naibu Waziri Mkuu wa kwanza nchini  Uganda Rebecca Kadaga, akiwaongoza Wabunge wa EALA,  kuzuru na kukagua ujenzi unaonedelea wa uwanja wa Arusha nchini Tanzania, alisema Viza moja itarahisisha usafiri wa mashabiki wataohudhuria mechi.

Kadaga ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa jumuia ya Afrika mashariki alisema Viza moja itachangia usafiri wa haraka na rahisi.

Mbunge wa EALA kutoka Tanzania, Abdullah Makame, aliongeza kuwa Viza moja itafungua fursa za kibiashara na kiuchumi  baina ya mataifa matatu ya Afrika mashariki wakati wa AFCON.

Uwanja wa Arusha umefikia asilimia 95 kukamilishwa ni mojawapo wa viwanja  sita vitakavyotumika kuandaa mechi za AFCON mwaka ujao .

Fainali za AFCON zitaandaliwa kati ya Juni 19 na Julai 17 mwaka ujao huku mataifa 24 yakishiriki.

Share This Article