Afisa mkuu mtendaji wa FIFA atimuliwa kwa kumkashifu Infantino

FIFA ililazimika kuweka kando mpango huo kufuatia shutuma kali kutika kwa mataifa wanachama huku wengine wakimtaka Infantino ajiuzulu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la kandanda ulimwenguni FIFA limempiga kalamu afisa wake mkuu mtendaji Kevin Lamour ,chini ya wiki tatu baada ya kumkashifu hadharani Rais Gianni Infantino kufuatia mpango uliotibuka wa kuuza hisa .

Lamour amekuwa afisini kwa miaka miwili katika wadhfa huo .

Kupigwa teke kwa Lamour kunatokea takriban mwezi mmoja baada ya kuutaja mpango wa FIFA kuuza hisa kuwa ‘mpango wa mtu mmoja’.

FIFA ililazimika kuweka kando mpango huo kufuatia shutuma kali kutoka kwa mataifa wanachama huku wengine wakimtaka Infantino ajiuzulu.

Share This Article