Miamba wa soka wa Tanzania, klabu ya Simba, wameafikiana kuachana na kocha mkuu Fadlu Davids baada ya kuhudumu kwa mmoja pekee.
Kulingana na taarifa kwa umma, usimamizi wa Simba umetaja hatua hiyo kuwa ya maafikiano kati ya timu na Fadlu baada ya raia huyo wa Afrika Kusini kutaka aruhusiwe kuondoka.
Fadlu anaaminika kuomba kusitisha mkataba na Simba baada ya kusajiliwa na miamba Raja Casablanca ya Morocco.
Akiwa Simba Fadlu ambaye ni raia wa Afrika Kusini aliwaongoza Simba kumaliza katika nafasi ya pili ligini na kucheza hadi fainali ya kombe la Shirikisho.