Mwigizaji wa filamu za Nollywood Esther Nwachukwu amesimulia jinsi uhusiano wake na mwigizaji mwenza Judy Austin uliharibika.
Nwachuku alichapisha picha za mawasiliano kati yake na Judy Austin ambaye ni mke wa pili wa mwigizaji Yul Edochie huku akimtaja kuwa mshirikina.
Alielezea kwamba yeye na Judy Austin, walikuwa marafiki hasa mitandaoni kutokana na maudhui yake ya kukosoa watu kadhaa maarufu nchini Nigeria.
Kulingana naye, Austin alikuwa akifurahia sana kila alipowakosoa mke wa kwanza wa Tul aitwaye May na shangazi ya Yul aitwaye Rita Edochie.
Wakati mmoja, Esther anasema aliunda maudhui ya kumkosoa mwanamuziki Davido kwa kutelekeza mtoto wake wa kwanza kwa jina Imade.
Maudhui hayo anasema yalimghadhabisha sana Judy Austin ambaye alimzomea kupitia jumbe na wakati huo ndio aligundua kwamba Judy hakuwa mtu mzuri.
Alishangaa ni kwa nini anafurahia May na Rita ambao hawajamkosea wakikosolewa mitandaoni lakini hataki Davido akosolewe kwa kutelekeza mtoto wake.
Sasa Esther Nwachuku anadai kwamba Judy Austin amemweka Yul Edochie kwenye chupa ndiposa marafiki zao wa Nollywood na wengine maarufu wameanza kuwatelekeza.
Anasema kwa sasa Judy ndiye anamtawala Yul Edochie kiasi cha kumfanya atelekeze May na watoto wake.