Kanye apeleka mzozo wa malezi kati yake na Kim mahakamani

Kanye anadai kwamba Kim Kardashian amekuwa akikiuka masharti ya makubaliano yao ya malezi na kutoheshimu haki zake kama mzazi mwenza wa watoto wao wanne.

Marion Bosire
3 Min Read

Kanye West ametoa malalamiko yake ya muda mrefu kuhusu Kim Kardashian kutoka kwenye macho ya umma na kuyapeleka mahakamani.

Mwanamuziki huyo wa mtindo wa Rapambaye pia ni mtayarishaji muziki na mfanyabiashara ametuma kile kinachoripotiwa kuwa barua halali ya kumzuia na kumkomesha mke wake wa zamani.

Kanye anadai kwamba Kim Kardashian amekuwa akikiuka masharti ya makubaliano yao ya malezi na kutoheshimu haki zake kama mzazi mwenza wa watoto wao wanne ambao ni North, Saint, Chicago na Psalm West.

Kulingana na ripoti barua hiyo ina orodha ndefu ya malalamiko ambayo Kanye anadai yamekuwa yakijijenga kwa miaka mingi.

Yanahusisha yeye Kutengwa na watoto wao na hata hofu kuhusu jinsi wanaonyeshwa kwa umma na sasa Kanye anataka kutambuliwa kisheria kwa malalamiko hayo na mabadiliko ya haraka kutoka kwa Kim.

Kuna pia utata wa kila mara kuhusu shughuli za mwanao North West kwenye mitandao ya kijamii.

Kanye kwa muda mrefu amekuwa akieleza wazi kwamba anapinga watoto wao kuwa kwenye majukwaa kama TikTok. Katika mahojiano ya zamani mwanamuziki huyo aliwahi kusema kwamba anaamini mitandao sio salama kwa watoto wadogo.

Barua hiyo ya kuzuia na kukomesha inamkabili Kim moja kwa moja kwa kuendelea kumweka North kwenye TikTok licha ya pingamizi za wazi za Kanye. Anaona hili kama dharau la makusudi kwa makubaliano yao ya malezi ya pamoja na matumizi mabaya ya mamlaka ya mzazi mmoja.

Kanye anasisitiza kwamba watoto wao hawapaswi kuonekana kwenye mitandao ya kijamii hasa yenye watumiaji wengi wanaoweza kuona na kuingiliana na maudhui yao. Anasema kuonekana huko kunaweka watoto wao kwenye mwanga wa umma usiohitajika.

Katika barua hiyo Kanye analalamikia pia tukio kwenye Met Gala ya 2025 ambapo anadai Kim alimwacha North peke yake kwa dakika chache wakati yeye alipojitokeza hadharani kwenye Red Carpet.

Kanye anadai kuwa kutokuwepo kwa Kim kwa muda huo kulimuweka North katika hali ya hatari na kumfanya aonekane kwenye vyombo vya habari bila uangalizi wa kutosha wa mtu mzima.

Anamlaumu Kim kwa kukosa busara kwa muda huo na kuliona kama mfano mwingine wa kipaumbele anachoweka kwenye taswira yake hadharani kuliko majukumu ya kuwa mzazi.

Ingawa maelezo ya kesi bado hayako wazi, shutuma ni nzito na zinaonyesha kuwa sasa Kanye anafuatilia kila hatua ya Kim anapokuwa na watoto wao.

Website |  + posts
Share This Article