EPRA yapunguza bei za mafuta

Tom Mathinji
1 Min Read

Halmashauri ya kudhibiti bidhaa za petroli hapa nchini EPRA, imetangaza kupunguzwa kwa bei za mafuta katika tathmini ya hivi punde.

Katika tangazo lake la Alhamisi, bei ya mafuta ya Petroli imepungua kwa shilingi tano, ile ya Diseli kwa shilingi mbili huku mafuta taa kwa shilingi nne.

Kupunguzwa kwa bei hizo za mafuta kunajiri siku chache baada ya kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement ODM Raila Odinga mwishoni mwa juma, kuitaka serikali kupunguza bei ya bidhaa za mafuta kwa kati ya shilingi 48 na 50.

Kulingana na Raila, bei ya mafuta katika soko la kimataifa imepungua.

Kwa sasa bei ya lita moja ya mafuta ya Petroli itauzwa kwa shilingi 212.36 Jiji Nairobi, diseli itauzwa kwa shilingi 201.47 huku mafuta ikiwa shilingi 199.05.

Jijini Mombasa lita moja ya bei ya Petroli itauzwa shilingi 209.3, diseli shilingi 198.41 na mafuta taa shilingi 195.92.

“Bei hizo zinajumuisha asilimia 16 ya ushuru wa dhamani kuambatana na sheria ya fedha ya mwaka 2023,” ilisema EPRA kupitia kwa taarifa.

Kulingana na EPRA, upungufu huo wa bei umetokana na kupungua kwa gharama ya usafirishaji.

Mabadiliko hayo yatadumu kwa muda wa mwezi mmoja.

TAGGED:
Share This Article