EPRA yaondolea mbali hofu ya kuwepo kwa mafuta duni nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya kudhibiti kawi na mafuta ya petroli ncini (EPRA), imeondolea mbali hofu ya kuwepo kwa viwango duni vya mafuta katika vituo vya kuuza petroli nchini.

EPRA imesema baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa ushirikiano na Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini (KEBS),kufuatia mamalamishi ya baadhi ya wakenya kuhusu kuwepo kwa mafuta ghushi ,imeendesha uchunguzi katika vituo kadhaa na kubaini kuwa madai hayo si ya kweli.

EPRA imethibitisha kuwa bidhaa zote za petroli zinazoagizwa humu nchini hupitia utathmini wa kiwango cha juu kuhakikisha yanaafiki viwango vya ubora.

Mamlaka hiyo pia imeongeza kuwa hakuna haja ya Wakenya kuwa na hofu.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *