Wizara ya Habari na Uchumi Dijitali imethibitisha kuwa imedhibiti udukuzi uliofanyiwa mtandano wa afisi ya msajili wa mashirika humu nchini maajuzi.
Katika taarifa kwa vyombo vya Habari Waziri William Kabogo, amesema kuwa habari zilizochapishwa na wadukuzi hao na data iliyotumika vibaya imeondolewa mtandaoni.
Wizara hiyo pia imefafanua kuwa huduma za usajili wa mashirika zilizoathirika na udukuzi huo, zimerejelea hali ya kawaida na deta yote katika afisi hiyo iko salama dhidi ya udukuzi wa siku zijazo.
Aidha, Waziri amesema kuwa wamemeimarisha usalama wa mitandaoni katika afisi zote za serikali na taarifa zote zimehifadhiwa kwa usiri unaohitajika kwa mujibu wa katiba ya Kenya ya mwaka 2010.
Waziri pia ameomba radhi wote walioathiriwa kutokana na udukuzi huo wa mitandao ya usajili wa mashirika.