EACC yawakamata watatu kwa wizi wa pesa za umma

Uchunguzi wa EACC umebaini kuwa pesa hizo zilitolewa kwenye akaunti hizo zikiwa pesa taslimu katika juhudi za kuficha ukweli.

Dismas Otuke
1 Min Read
Makao Makuu ya EACC.

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini (EACC) imewakamata washukiwa watatu kuhusiana na wizi wa pesa za umma shilingi milioni 92.05.

Watatu hao walikamatwa kuhusiana na pesa hizo zilizotoka kwa kaunti ya Turkana kati ya mwaka 2013/2014 na 2024/2025.

EACC imebainisha kuwa kampuni mbili zilipokea malipo ya  jumla ya shilingi milioni 92.05 kutoka kwa serikali ya kaunti ya Turkana.

Tume ya EACC inachunguza kisa hicho ambapo pesa hizo zilitumwa katika akaunti mbili tofauti za benki. Akaunti ya kwanza ikipokea shilingi 62.04 kutoka kwa kaunti na akaunti ya pili ikapata shilingi miliobi 30.01 baada ya kupata kandarasi tano kutoka kwa kaunti ya Turkana.

Uchunguzi wa EACC umebaini kuwa pesa hizo zilitolewa kwenye akaunti hizo zikiwa pesa taslimu katika juhudi za kuficha ukweli.

Watatu hao waliokamatwa Jumatano walitarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kupambana na ufisadi mjini Eldoret mapema leo Alhamisi.

Aidha, tume hiyo imewataka watu wengine watano wanaohusishwa na uchunguzi huo kujisalimisha kwa afisa zake mjini Eldoret.

TAGGED:
Share This Article