Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali anayeondoka Dkt. Margaret Ndung’u amedinda uteuzi wa kuwa Balozi wa Kenya nchini Ghana.
Dkt. Ndung’u amesema hatua yake inatokana na sababu za kibinafsi.
Waziri huyo aliyeshikilia wadhifa huo kwa takriban miezi minne pekee alitarajiwa kupigiwa msasa na Kamati ya Ulinzi ya Bunge la Kitaifa leo Ijumaa.
Dkt. Ndung’u aliondolewa kwenye wadhifa huo katika mabadiliko ya hivi punde ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais William Ruto.
Wadhifa wake umekabidhiwa Gavana wa zamani wa kaunti ya Kiambu William Kabogo.
Kabogo aliteuliwa kumrithi Dkt. Ndung’u wakati Mutahi Kagwe akiteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Dkt. Andrew Karanja huku Lee Kinyanjui akiteuliwa kuwa Waziri wa Biashara.
Dkt. Karanja ameteuliwa kuwa Balozi wa Kenya nchini Brazil na amesailiwa leo Ijumaa asubuhi.