Nyumba milioni 1 kuunganishiwa umeme miaka 3 ijayo, asema Rais Ruto

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto amesema nyumba milioni 1 zitaunganishiwa umeme katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. 

Akizungumza leo Ijumaa katika kaunti ya Uasin Gishu kwenye siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu katika eneo North Rift, Rais Ruto alisema serikali yake inawekeza shilingi bilioni 1.8 ili kuunganisha umeme kwenye nyumba 20,000 katika kaunti hiyo katika kipindi hicho cha miaka mitatu.

Ili kudhihirisha hilo, Mzee Simeon Nyango na Mama Salina Nyango walikuwa na kila sababu ya kutabasamu baada ya kuunganishiwa umeme chini ya mpango wa kuunganisha umeme vijijini.

Akiwa katika eneo la Kesses, kaunti ya Uasin Gishu, Rais Ruto pia alizindua mradi wa kuunganisha umeme katika kijiji cha Cheboror.

Chini ya mradi huo, nyumba 316 zitaunganishiwa umeme.

Rais Ruto amewataka wakazi kuepukana na uongo na porojo zinazosambazwa na watu anaosema wana lengo la kuhujumu maendeleo ya nchi.

Aidha, ameonya dhidi ya siasa za mapema akiongeza kuwa ni mapema mno kuanza kuzungumzia uchaguzi wa mwaka 2027 na kutaka kipaumbele kuelekezwa kwa miradi itakayowanufaisha wananchi.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *