Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu (KNCHR), imemteua Dkt. Mary Kimari kuwa Afisa Mkuu Mtendaji, baada ya kukamilika kwa mchakato wa uajiri uliokuwa na ushindani mkali.
Dkt. Kimari anachukuwa wadhifa ulioshikiliwa na Dkt. Bernard Mogesa, tangu mwaka 2017.
Kupitia kwa taarifa, mwenyekiti wa KNCHR Claris Ogangah, alisema uteuzi wa Kimari, ulitekelezwa kwa njia ya uwazi, na ulizingatia katiba na sheria za tume hiyo.
Dkt. Kimari anatarajiwa kuongoza sekretarieti ya tume hiyo, pamoja na kufanikisha juhudi za kuimarisha uwezo wa tume hiyo kuboresha upatikanaji wa haki, na kuleta uwajibikaji kwa wanaokiuka haki za binadamu.
Majukumu mengine ya afisa huyo ni pamoja na kuleta mabadiliko kwenye sera na kuongeza uhamasishaji kuhusu haki za binadamu.
Uteuzi wa Kimari umejiri, huku KNCHR ikiendelea kupigia darubini utekelezaji wa haki za binadamu, uchunguzi wa malalamishi, na kuchocheabulinzi wa haki za kimsingi.
Wadhifa uliwavutia watu 138, waliojumuisha wanaume 102 na wanawake 36, huku watano wakiwa wale walio na ulemavu.
Hata hivyo ni watu tisa waliorodheshwa kusailiwa kwa wadhiwa huo, akiwemo Dkt. Kimaru.